Mchezo wa jana [NEWCASTLE UTD V/s PSG] zote zina wawekezaji wakubwa, PSG inamwekezaji kutoka Qatar ambaye tayari akuwa na timu kwa kipindi kisichopungua miaka 10 wakati Newcastle United imekuwa chini ya mwekezaji kutoka Saudi Arabia kwa miaka miwili sasa.
Mwekezaji wa PSG aliamini katika majina makubwa/ma-star na kuwaweka pamoja akiamini watampa anachokitaka na kumfikisha nchi ya ahadi lakini mwekezaji wa Newcastle United yeye ameamini katika kutengeneza timu itakayoshindana na sio kutengeneza timu kupitia mchezaji mmojammoja.
Mara ya mwisho Newcastle United kucheza UEFA Champions League ilikuwa msimu wa 2002|2003, jana ilikuwa ni sherehe kubwa kwao baada ya kupata ushindi mnono [Newcastle 4-1 PSG] ushindi uliotokana na ubora wa Newcastle United.
Kwa hiyo nilichokiona kwenye mchezo huu ilikuwa ni mechi kati ya timu dhidi ya kikundi fulani cha watu na hiyo ndio ilikuwa tofauti. Ushindi wa Newcastle United haukuwa wa kubahatisha, kuichapa mabao manne PSG haitokei kwa bahati.
0 Comments