Hot Posts

6/recent/ticker-posts

HISTORIA YA SOKA LETU: YANGA ALIWAHI KUAZIMA WACHEZAJI WA SIMBA KUCHEZA LIGI YA MABINGWA AFRIKA


Yanga, Dar es Salaam 1998. (KUMBUKIZI)

➡️Hii Yanga ya 1998 ilipoazimwa jezi na Taifa Stars na baadhi ya wachezaji wa Simba (3) kwenye mchezo wa wake wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kundi B dhidi ya ASEC Mimosa ya Ivory Coast.

➡️Mchezo ulichozwa Nov 8, 1998 ambapo kikosi ya Yanga kiliazimwa wachezaji watatu kuisaidia Yanga, licha hivyo basi Yanga ikafa 3 - 0 kwenye dimba ya Taifa (sasa Uhuru) Dar es Salaam. 

➡️Kutoka kulia waliosimama ni Salvatory Edward, Banza Tshikala, Edibily Lunyamila, Manyika Peter, Idelphonce Amlima, Alphonce Modest (Simba). 

➡️Waliochuchumaa kutoka kulia ni Monja Liseki (Simba), Mohammed Hussein ‘Mmachimba’, Shaaban Ramadhan (Simba), Mzee Abdallah ‘National’ na John Bocco Mwansasu.

➡️Wananchi walilazimika kuvaa jezi za Taifa Starts kutokana na jezi zao pekee za rangi ya njano, kufanana za mgeni. 

#Credit: Binzubeiry



 

Post a Comment

0 Comments