Hot Posts

6/recent/ticker-posts

MZIZE WA YANGA ATOBOA SIRI YA UBORA WAKE


Mshambuliaji kinda wa Yanga, Clement Mzize amefichua mambo mawili yanayombeba kwenye kiwango chake ni msimu huu ndani ya timu yake.

Mzize mwenye mabao matano hadi sasa amesema jambo la kwanza ambalo limemuongezea ubora ni mafunzo na maelekezo anayoyapata kwa kocha wao msaidizi Mussa Nd'aw ambaye ni mshambuliaji hatari wa zamani.

Moussa N'Daw ni Mwanasoka wa zamani wa Kimataifa wa Senegal, ambaye alikuwa mshambuliaji hodari enzi zake na alichezea klabu nyingi ikiwemo Wydad Casablanca ya Morocco,Al-Hilal ya Saudí Arabia, Farense ya Ureno na Al-Ittifaq.

"Amekuwa akinijenga sana, ni kocha ambaye ana vitu vingi bahati nzuri na yeye alicheza nafasi kama yangu tena kwa mafanikio makubwa kila wakati amekuwa akinikosoa na kunielekeza Cha kufanya,"amesema Mzize.

"Kuna mbinu nyingi amekuwa ananiongezea pia jinsi ya kuwakabili mabeki wa timu pinzani, nimekuwa napata msaada mkubwa kwa makocha wangu mazoezini na hata kwenye mechi.

Aidha Mzize ameongeza kuwa mbali na mafunzo hayo kutoka kwa kocha wake pia amekuwa na ratiba binafsi ya kufunga wanapomaliza mazoezi ya timu nzima au kabla.

"Kuna ratiba binafsi pia huwa nafanya mara nyingine nimekuwa nikifanya na washambuliaji wenzangu au hata viungo au mabeki wananitengenezea nafasi na mimi natakiwa kufunga hiyo tunafanya sana kabla ya mazoezi kuanza au yanapomalizika.

"Nilichojiwekea malengo ni kwamba iwe nimepata nafasi ya kuanza au kuingia nikitokea benchi basi lazima nifanye kitu cha kuisaidia timu kama sio kufunga basi hata nitengeneze nafasi mwingine afunge."

 

Post a Comment

0 Comments