Siku zote ubora wa timu hua unaanzia chini kwa maana ya ukuta, golikipa pamoja na mabeki kisha tunakuja katika eneo la kiungo
Na ikitokea eneo hilo kuna shida mahala basi huwezi kuupata ubora wa wachezaji wengine kwa maana ya washambuliaji na kuipa timu balance nzuri ya kupata matokeo chanya
Ukikitazama kikosi cha Simba SC kinammis zaidi Tanzania One Aishi Salum Manula @28_manula , hapa lazima tuuseme ukweli, amekuwa muhimili mkubwa na kuiweka salama wakati wote timu na kuwafanya Wachezaji wacheze kwa kujiamini
Ubora na uzoefu wake uliendelea kuipa uimara Simba na hata mashabiki kutembea kifua mbele wakiamini wanaye mtu atakayeilinda milango na wao kufanikiwa zaidi
Naam, jambo jema ni Aishi Manula amesharejea kwenye kikosi na anaendelea na mazoezi ya kuuweka mwili fiti baada ya kukosekana kwa muda kidogo
Sitotoshi kiwango cha Ayoub, hapana na siyo lengo langu lakini hata hivyo ugeni wake katika kikosi cha Mnyama nalo ni sababu ya kufungwa magoli yenye ukakasi
na kutilia shaka ubora wake
Ayoub amekuwa akifungwa magoli ya Kibinadamu sana na hata wakati mwingine unatamani kumpa jezi Manula akaitetee gloves 🧤 ya Simba kipindi ambacho mashabiki wanahitaji timu ishinde ili wakatambe huko waishiko
Yes tuendelee kuiombea @simbasctanzania lakini tuzidi kupiga Dua kwa Tanzania One Aishi Salum Manula arejee haraka kwani kuna michuano ya Super Cup Afrika itaanza siku si nyingi
Haya ni maoni yangu naomba yachukuliwe kama yalivyo 🙏
0 Comments