Hot Posts

6/recent/ticker-posts

YANGA NA MFUPA MGUMU ULIOWASHINDA WENGI AFRIKA


Klabu ya Yanga ya Tanzania ndani ya miaka hii miwili katika michuano ya Afrika imeanza kutengeneza rekodi ya kutisha dhidi ya timu nyingine zinazoshiriki michuano ya ngazi za vilabu Afrika.

Mfupa mgumu katika michuano hii ya vilabu barani Afrika ni kushinda ugenini jambo ambalo katika hali ya kawaida haliwezi kutokea kirahisi bila kujali ubora wa timu zinazokutana.

Mfupa huu mgumu ambao umekuwa desturi Kwa miaka kadhaa na Kwa vilabu vikubwa Afrika unaonekana kupata dawa yake ambayo ni klabu ya Yanga kutoka Tanzania.

Msimu uliopita katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika, Yanga walishinda mechi ngumu za ugenini huku wakitawala mechi hata katika zile mechi ambazo hawakushinda Kwa maana ya kufungwa au kudroo.

Yanga walishinda dhidi ya Rivers United nchini Nigeria 2-0, walishinda dhidi ya Club Africain nchini Tunisia 1-0, wakashinda dhidi ya TP Mazembe nchini DR Congo 1-0, wakashinda dhidi ya Marumo Gallants 2-1 nchini Afrika Kusini, wakadroo dhidi ya Real Bamako 1-1 nchini Mali na pia wakashinda 1-0 dhidi ya USM Alger nchini Algeria.

Mechi ya jana ya ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya El Merreikh ni muendelezo wa vitisho ambavyo Yanga inavitoa Kwa kuwapiga 2-0 nyumbani kwao na kutuma salamu Afrika kuwa ule mfupa mgumu umepata mbabe wake.

Kwa jinsi Yanga inavyocheza hasa mechi za ugenini ni habari mbaya Kwa vilabu vingi barani Afrika na hii inaweza kuwafikisha yangu katika hatua kubwa sana msimu huu katika michuano ya ligi ya mabingwa Afrika msimu huu.

 

Post a Comment

0 Comments