Kama kuna kitu ambacho Simba ilipatia ni uamuzi mzuri wa uteuzi wa kikosi cha kwanza uliofanywa na Kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’. kocha huyo alipatia kila kitu. Moses Phiri ni Mzambia. Mpinzani alikuwa Mzambia.
Phiri ni moja kati ya washambuliaji wenye kila kitu. Kumuanzisha ulikuwa uamuzi sahihi, lakini dakika 45 za kwanza ni kama alikuwa mtalii uwanjani. Hakukuwa na presha kubwa kutoka kwake kwenda kwa mabeki wa Dynamos.
Ni kama dakika 45 zote alikuwa anarukaruka tu uwanjani. Washambuliaji wana faida moja tu kubwa. Anaweza kucheza ujinga kipindi cha kwanza, lakini akafunga kipindi cha pili na kuwafuta machozi mashabiki. Mchezaji kama Phiri alipaswa kufanya makubwa kipindi cha kwanza.
Kelele zimekuwa nyingi sana juu yake. Mashabiki wengi wa Simba wanadhani kocha huwa anambania kwa kumuweka benchi. Wengi wanaamini ana uwezo mkubwa. Ana uwezo wa kuibeba Simba. Mechi kama hizi mara zote ndizo ni za kutengeneza heshima. Mechi za kutengeneza imani kwa kocha na mashabiki. Simba na Yanga huwa hazina uvumilivu wa muda mrefu. Ni aina ya timu zinazotaka matokeo chanya mapema.
Kwa dakika 45 za kwanza, kiukweli Moses Phiri amewaangusha Msimbazi. Alikuwa anarukaruka tu. Najua na wewe ulitazama mechi, naomba maoni yako 👇
0 Comments