Hot Posts

6/recent/ticker-posts

DJUMA SHABAN AMZINDUA CHILAMBO AZAM FC


Beki wa kulia wa Azam FC Nathaniel Chilambo amesema Kwa Sasa anapambana kuhakikisha anapewa muda mwingi wa kucheza. Hivi karibuni uwanja wa Azam Complex, Chamazi alionekana mchezaji wa zamani wa Yanga Djuma Shaban akifanya mazoezi na kucheza mechi za kirafiki na timu hiyo na huenda akasajiliwa katika dirisha dogo.

Chilambo amesema amejiandaa kufanya juhudi na kujituma zaidi ili kumuonesha kocha anaitaka namba kikosi cha kwanza. Ushindani wa namba umemfanya apate dakika chache mbele ya beki mwenzie Lusajo Mwaikenda ambaye ameonekana kufanya vizuri na kuiteka nafasi hiyo.

"Najua kinachoendelea lakini kwangu nafanya juhudi zangu na kujituma mazoezini na kwenye mechi ili nizidi kumuonesha kocha kuwa naitaka namba". Amesema Chilambo.

 

Post a Comment

0 Comments