Manchester United wameweka hadharani kupitia mitandao yao ya kijamii wachezaji 25 ambao watawatumia kwenye ligi kuu ya England 2023/24.
Majina ya nota wapya kwenye kikosi ikiwemo Mason Mount, Andre Onana, Altay Bayindir, John Evans na wale ambao wapo kwa mkopo Sofyan Amrabat a Sergio Reguilon wamejumuishwa kwenye idadi ya wachezaji 25.
Cha kushangaza zaidi kwenye wachezaji hao 25 hakuna jina la usajili mpya wa Manchester United kutokea Atlanta Rasmus Hoilund na Alejandro Gernacho ambaye ni mmoja ya wachezaji muhimu kwenye kikosi cha Manchester United.
Machaguo ya nyota hao 25 yamezingatia wale ambao wapo juu ya miaka 21. Kulingana na sheria za ligi kuu ya England wachezaji ambao wamezaliwa January 1 mwaka 2002 au baada ya hapo hawaruhusiwi kusajiliwa kwenve timu hivyo watatumika kama wachezaii wa chini ya miaka 21.
Na hii ndio sababu Rasmus Hoilund na Gernacho hawajajumuishwa kwenye list ya wachezai 25 ambao Manchester United imewasajili kwaajili ya ligi kuu ya England msimu huu.
0 Comments