Katika orodha hiyo hakuna hata mwamuzi mmoja kutoka Tanzania! Lakini majirani zetu Kenya, Rwanda, Burundi, DR Congo, Somalia na Sudan waamuzi wao wamechaguliwa.
Mwenyekiti wa Chama cha Waamuzi Tanzania Nassoro Hamduni amesema, waamuzi wa Tanzania wana sifa na vigezo vya kuchezesha mashindano ya CAF ndio maana wamekuwa wakiteuliwa kuchezesha mechi za Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho.
“CAF ndio wanateua, wameona hao ndio wanafaa na nafasi ni chache kwa hiyo kutokuwepo sisi imetokea kwa sababu sio eneo letu sisi, CAF ndio wenye mashindano na ndio wanaamua wanahitaji waamuzi gani.”
“Ni nafasi tu na waamuzi wakijaa basi, waamuzi wa Tanzania vigezo wanavyo na wapo ambao wameteuliwa kuchezesha mashindano ya CAF wiki hii! Kama wangekuwa hawana vigezo wasingeteuliwa.”
Takriban waamuzi 69 [wamuzi wa kati, wasaidizi na wataalam wa VAR] wameteuliwa na CAF.
0 Comments