ahmedabdallah05 anaandika .....
Kosa moja halihalalishi kosa lingine, ni kweli jana katika mchezo kati ya Yanga na Namungo ilipaswa kutoka adhabu kali kwa rafu aliyochezewa Lomalisa jambo ambalo lilipaswa kuhakikishwa na mwamuzi mwenye dhamana ya kusimamia sheria za soka uwanjani.
Ni uhalisia wa zama na zama kwa mashabiki wa Simba na Yanga kuombeana mabaya, lakini mabaya hayo ni kwa level ya ushindani tu na sio kufika mpaka kwenye level ya kibinaadamu, Yaani jana Mnyama alitaka hasimu wake akaziwe na Namungo na vivyo hivyo leo Wananchi walitamani Coastal Union wafanye jambo la kuwafurahisha.
Pale uwanjani Wachezaji wanakuwa katika eneo lao la kazi ni kama mimi na wewe tunapotoka nyumbani na kwenda kazini kutafuta rizki, kwa chochote kibaya kitakachomtokea kwa kuchezewa rafu mbaya itakayoathiri kitendea kazi ambacho ni mwili wake basi ni dhahiri kinaweza kusitisha ajira yake.
Rafu aliyoifanya Haji Ugando Kwa Henock Inonga leo ni kawaida hutokea kwenye mchezo wa soka na ukimuuliza Ugando sasa hivi anaweza akawa anajuta na asingependa kufanyiwa yeye.
Lakini cha ajabu kuna baadhi ya watu wamefurahia kilichomkuta Inonga wakisema ilikuwa nyepesi sana mbona jana haikutoka kadi nyekundu lakini pia wanakumbusha kuwa Inonga hakuadhibia alipomchezea rafu Babu Kaju kwenye mchezo kati ya Simba na Yanga, kama nilivyosema awali kosa moja halihalalishi kosa lingine yote ni makosa ambayo waamuzi walipaswa kuwawajibisha waliotenda.....
0 Comments