Goli la kwanza la Bayern Minich kwenye mchezo wa jana dhidi ya Manchester United [Ligi ya Mabingwa Ulaya] lilionekana kuwavunja nguvu wachezaji wa Man United kwa namna ambavyo lilifungwa, kuanzia golikipa mwenyewe Onana ambaye ndio alifanya makosa hadi wachezaji wengine wote!
Goli lililofungwa kutokana na makosa ya Onana lilifanya wachezaji waone kazi yote ya kuzuia waliyoifanya kwa dakika zote kabla ya goli iwe ni sawa na bure tu.
Onana anapitia wakati mgumu sana kwa sasa na hii ndio inathibitisha De Gea alikuwa golikipa mzuri. Manchester United inashambuliwa sana, hata kama kipa anafungwa haiondoi ubora alionao.
Onana anafikiwa sana, anaokoa hatari nyingi na mwisho wa siku unakuta zile hatari ambazo alistahili kuokoa ndizo anafungwa na zile ambazo unakuta anakutana uso kwa uso na mshambuliaji anaokoa!
Kwa hiyo kufikiwa mara kwa mara kunasababisha wakati mwingine afanye makosa ambayo hata wachezaji wengine wanafanya ndani ya uwanja.
Kuna kipa anaweza akafungwa halafu anaenda kuchukua mpira nyavuni ili watu wakanze kwamba tayari tukio limepita na inabidi kuendelea na mchezo, lakini Onana akifungwa ni mpaka mtu akamwinue. Hata kama goli alilofungwa hakuwa na namna ya kuzuia lakini utaona anajutia sana kufungwa.
- Amri Kimemba, Mchambuzi Clouds Media.
0 Comments