Licha ya ushindi mzuri lakini ukiwauliza mashabiki wengi wa Simba SC bado hawaridhishwi na namna safu ya ushambuliaji ya timu yao inavyopoteza nafasi.
Wengi wanaamini timu inatengeneza nafasi nyingi ambazo hazitendewi haki. Idadi ya magoli yanayofungwa na idadi ya nafasi zinazotengenezwa hazina uwiano.
Hii ni kweli kwani kuanzia mechi dhidi ya Dodoma Jiji, Power Dynamos na hii ya leo idadi ya nafasi zinazotengenezwa ni nyingi ukilinganisha na mabao yanayofungwa.
Simba SC wanatakiwa kuwa wakatili sana kwenye kufunga kwasababu zipo mechi ambazo nafasi zitakuwa ni nadra kupatikana na mechi zitakuwa ngumu kwao.
Licha ya ushindi mzuri na mkubwa lakini nimechagua kuuongelea upande dhaifu wa Simba kuliko kusifia...
Nani atamzuia Chama asipige miasist??... Nani atamzuia Baleke asifunge??...
SIMBA SC 3-0 COASTAL UNION
Baleke⚽⚽⚽
Simbaaaaaa🔥🔥
0 Comments