-Kuna utofauti kati ya mchambuzi na shabiki. Shabiki anaweza kufanya kitu kwa mihemko lakini mchambuzi unapaswa kuepuka kufanya vitu kwa mihemko au kuingiza hisia zako binafsi.
Kwenye uchambuzi jaribu kutoa hoja ambazo hata mtu akizisoma au kuzisikia anaona utofauti kati yako na shabiki.
Nimeona mjadala baada ya mchezo wa jana kati ya Power Dynamos na Simba, baadhi ya ndugu zangu wanaitumia kama hoja ya kujustify kwamba Zimbwe na Kapombe wamechoka.
Sipingi mtazamo wao lakini napinga hoja wanazotumia kutuaminisha kuwa wawili hao nyakati zimewatupa mkono.
Hoja ya kutumia bao la kwanza la Power Dynamos kama sababu ya kusema Kapombe amechoka kwa mtazamo wangu haina mashiko kwa vile lilitokana na makosa ya kiujumla ya safu ya ulinzi ya Simba.
Kapombe huwezi kumlaumu kwa vile kati yake na Mutale ilikuwa ni situation ya 1v1. Situation ya 1v1 huwa ni ngumu kwa walinzi wengi sio Kapombe tu bali duniani kote hasa kunapokuwa na winga mbunifu kama Mutale. Na ndio maana makocha wengi wanaojielewa husisitiza timu zao kutoruhusu kutokea kwa situation ya 1v1.
Pale tunamsifu zaidi Mutale kwa ubora wake na sio Kapombe.
Hoja dhaifu kabisa ni ile ya Zimbwe kwamba kutolewa kwake juzi ni kwa sababu alichoka.
Kwa mwenye uelewa wa mpira wa miguu, kutolewa kwa Zimbwe ilikuwa ni mabadiliko ya kiufundi (technical substitution) na sio kwamba Tshabalala alichoka.
Muda ule Simba ilikuwa inaongozwa kwa mabao 2-1, beki wa kati wa timu pinzani amepata kadi nyekundu, kocha yeyote mwenye akili timamu, atahitaji kuwa na namba kubwa ya washambuliaji sasa mlitaka Robertinho atoe mshambuliaji ili aingie mshambuliaji?
Ilikuwa simple tu, unatoa beki au kiungo wa ulinzi ili kuongeza namba ya washambuliaji mbele na hicho kiliipa Simba mafanikio.
Hili hata shabiki wa kawaida mbona ameelewa inakuaje ngumu kwa mchambuzi kuelewa?
Kapombe na Zimbwe wahukumiwe kwa hoja za haki na zenye mashiko na sio nyepesi na za kimihemko
0 Comments