Siku moja nilimfuata @alikamwe nikamuuliza hivi hawa wachezaji wanaoondoka itakuwaje?
Kamwe akaniambia hebu twende kwa @caamil_88 tumsikilize. Kufika ofisini mwamba hakuonekana hana wasiwasi ndio kwanza anatabasamu kutokana na maswali yetu
Akasema kuwa wadogo zangu mimi ni kaka yenu msiogope, nipo mbele yenu niwe mfano kwenu. Kila nafasi iliyoachwa wazi itazibwa maradufu kimfumo.
Nikabaki na maswali mengi, inakuwaje hana hofu?katika nyakati ambazo tunaona ni ngumu na zenye maswali tata kwake ni tofauti kabisa.
Juzi wakati tupo njiani kwenda Rwanda akampigia simu Ally Kamwe akamwambia mkifika Rwanda njooni moja kwa moja na mashabiki uwanjani.
Alitusubiri kwa takriban masaa matano, tulipofika uwanjani akawaambia mashabiki kuwa nitanunua tiketi zote, nikawaza kwa mfano wakifika mashabiki 2000 si hela nyingi sana?
Ni kweli uwanja ulijaa, tiketi takribani 2000 zenye thamani ya Tsh 50m.
Ee bhana Mimi mchaga kwanza iliniuma kuona tunapeleka milion 50 kwa mpinzani wetu El Merrikh. Kabla sijafika hoteli nikampigia Nikamuuliza Injinia tukifungwa na hela tumewapa itakuwaje? Huon kama tutakuwa tumepata hasara mara mbili? Bora hata hasara ya mechi pengine tutashinda nyumbani, vipi hiyo milion 50? Injinia akacheka akaniambia kapumzike mdogo umechoka na safari.
Kesho yake sikukata tamaa nikamuuliza tena, Akaniambia mdogo wangu, mafanikio yanatokana uthubutu. Nikamwambia hiyo ni risk akanimbia kwenye vita hakuna riziki kuna risk twende vitani mdogo wangu.
Aakanikumbusha msemo wa Berluscone alisema mpira wa miguu ni sawa na mwanamke mzuri sana, na siku zote ukitaka kuishi kwa amani na mwanamke mzuri mgharamikie. Hata kwenye maandiko imeandikwa
Injinia ameonesha hili kwa vitendo, Kwanza ameugharamikia mchezo kuhakikisha mashabiki wanajaa uwanjani, pili ukitaka kujua anajali, licha ya kutoa fedha nyingi aliamka mapema saa 12 na kwenda kushughulikia suala la tiketi. Hakwenda kula lunch, majira ya saa 7 mchana alishinda juani kwenye geti la uwanja kusubiria mashabiki na kuwapokea
Baada ya mechi akaniuliza mchaga vipi umeelewa fumbo langu kwako? Nikamjibu kwenye alama za nyayo zako umeacha miba kama mtu hana uthubutu na ujasiri hawezi kupita
0 Comments