Hot Posts

6/recent/ticker-posts

TUNAIOGOPA SANA MAMELODI SIO SIMBA

Baada ya Simba SC kupangwa na Al Ahly kwenye robo fainali ya michuano ya African Football League, mchezaji na kocha wa zamani wa Al Ahly Mokhtar Mokhtar amesema mechi wanayoiwazia ni dhidi ya Mamelodi Sundowns na sio Simba. 


Mshindi wa mechi ya Robo Fainali ya Simba na Al Ahly atakutana na mshindi wa robo fainali ya Mamelodi Sundowns na Petro de Luanda kwenye hatua ya nusu fainali. 


“Simba ndio wanatakiwa kuhofia kukutana na Al Ahly,ila mimi ninahofia kukutana na Mamelodi Sundowns” —Amesema Mokhtar kupitia mtandao wa Kingfut. 


“Al Ahly wanaweza kuifunga timu yoyoye Afrika, lakini hesabu zetu mara zote hubadilika tunapokutana na Sundowns” aliongeza.
 

Post a Comment

0 Comments