Hot Posts

6/recent/ticker-posts

KOCHA WA CHELSEA AAMBIWA ABADILI MFUMO


 Mashabiki wa Chelsea maarufu kama ‘The Blue Army’ wamemtaka kocha Mauricio Pochettino kubadili mbinu za uchezaji haraka. Mashabiki wanaamini mabadiliko yakifanyika wataweza kushinda mchezo wao ujao dhidi ya Bournemouth.

.

Mashabiki sasa wanamtaka Pochettino afanye mabadiliko, huku shabiki mmoja akipinga uwepo wa beki Thiago Silva na uteuzi wa fomesheni inayochezwa. Chelsea imekuwa ikitumia mabeki wa tatu na mashabiki hao wanataka warudi kwenye utamaduni wao wa kutumia mabeki wanne.

.

Mfumo wa sasa unamfanya beki wa kushoto Ben Chilwell kuchez wingi ya kushoto, huku beki wa kati mpya, Levi Colwill akicheza upande wa kushoto. Hilo linafanyika wakati mawinga wa asili Mykhailo Mudryk na Noni Madueke wakiendelea kusugua benchi. Na hata Axel Disasi mashabiki wanadai hatumiki ipasavyo.

Post a Comment

0 Comments