Hot Posts

6/recent/ticker-posts

TAIFA STARS NA ALGERIA GAME ITAKUWA NGUMU SANA

Inawezekana kuna watu wanaamini mchezo wa Algeria vs Tanzania kufuzu Fainali za AFCON utakuwa mwepesi kwa Tanzania kwa sababu Algeria tayari imeshafuzu kwa hiyo haina kitu cha kupoteza kwenye mchezo huo. Jibu ni HAPANA!

Mechi hiyo ina umuhimu mkubwa kwa mataifa yote mawili [Algeria na Tanzania], ni mchezo muhimu kwa Algeria kwa sababu ya kuendelea kujenga timu, Kocha kuendelea kuchagua wachezaji wa kwendanao kwenye Fainali za AFCON nchini Ivory Coast.

Lakini pia Kocha wa Algeria anaweza kuwa anataka kuweka rekodi kwa sababu makocha nao ni washindani na wanapenda kutengeneza vitu vyao na kuacha alama. Anaweza akawa anataka kuweka rekodi ya kucheza mechi za kufuzu AFCON bila kupoteza mchezo.

Ndio maana makocha wengine wakifanikiwa sana wakiwa na timu fulani wanaondoka hawataki kuendelea kwa sababu hawataki kuharibu CV walizotengeneza na wanaamini itaendelea kuwapa kazi kwenye maeneo mengine.

Kwa hiyo mechi ya kesho inaweza kuwa ni muhimu zaidi kwa Kocha wa Algeria kuliko namna ambavyo mashabiki wanaitazama.

Kama Kocha atafanya mabadiliko ya kikosi kwa kuwapa nafasi wachezaji ambao huwa hawapati nafasi mara kwa mara itaongeza umuhimu wa mechi kwakuwa watataka kumshawishi kocha kitu gani wanaweza kufanya.

Baomdo naona ni mechi muhimu kwa timu zote mbili japo timu moja [Algeria] matokeo yoyote hayataathiri kile ambacho tayari wanacho.


 

Post a Comment

0 Comments