GOOD NEWS KUHUSU BAKA
Daktari Richard Jomba wa Simba sc amewatoa wasi wasi Mashabiki na wanachama wa Simba kuhusu Hali ya Beki wao Inonga Baka ameelezea hali ya jeraha hilo kwamba ni la Kawaida sio Kubwa kama ilivyokuwa inadhaniwa Mwanzoni
🗣️“Kwa ujumla mpaka sasa hivi kwa hatua hii mpaka natoka, hali yake ni nzuri na jeraha lake sio kubwa, ni dogo na vitu vyote vimeshafanyika na yuko vizuri, sasa yupo kwenye mapumziko mafupi na ataruhusiwa kutoka hapa hospitali.”
“Kwa vipimo vya haraka haraka alivyofanyiwa sidhani kama atakaa nje kwa muda mrefu, kilichobakia ni kuuguza sehemu ya kidonda Kwa hiyo atakuwa na muda wa kuuguza ile ngozi ile sehemu ya kidonda lakini si vinginevyo.”
0 Comments