Hot Posts

6/recent/ticker-posts

TARAAATIBU SIMBA WANAANZA KUJIPATA LIGI KUU

 


🖋 kenny_Mchambuzii


Simba SC leo katika Dimba la Uhuru wametujibu kwa vitendo baada ya kushinda ushindi mnono na pira kubwa "Umiliki wa Mpira asilimia 87 kwa Mnyama,13 kwa Coastal Union.

.

Katika michezo ya nyuma wamekua wakipata ushindi katika mazingira magumu lakini leo wamebadilika kwa kiasi kikubwa tumeliona SAMBALOKETO na umiliki wa Mpira ukiwa mkubwa kwa upande wao.

.

Mbinu na mipango ya Simba SC leo ilikua thabiti katika kipindi cha kwanza huku wakicheza kwa kujituma na kucheza soka linalovutia.

.

Coastal Union kipindi cha kwanza walifanya baadhi ya makosa yaliyowapelekea Simba SC kutumia vyema huku Haji Ugando akapata kadi Nyekundu ikawatoa mazima mchezoni katika kipindi cha kwanza .

.

Kipindi cha pili Vijana wa Mwinyi Zahera wakaingia tofauti,wakionyesha uhai katika eneo la katikati mabadiliko waliyofanya yamewasaidia na wakiongeza nidhamu,tahadhari na kujituma na kupunguza idadi ya magoli.

.

Clatous Chota Chama "WHAT A PLAYER " Mpira unamtii sana,alikua engine ya Mnyama katika siku ya leo na kuufanya mchezo kuwa mkononi mwake,kawapa wakati mgumu sana Coastal Union. 

.

Jean Baleke "MR HATTRICK " katia tatu kambani,anakaa vyema kwenye nafasi na utulivu wake umemfanya kukwamisha vyema mpira kambani,magoli haya yanamfanya kuwa kinara (kafikisha magoli 5).

.

Che Malone "Ukuwa wa Jericho " Mlinzi kisiki,amekua na siku bora kazini,alikua akisahisha na kukaba vyema huku wakisaidiana vyema na walinzi wenzake na kuifanya lango lao kuwa salama na kupata CLEAN SHEET.


NB.SIKU MTU AKIPIGWA 10 NDIO MTAIHESHIMU LUNYASI 😃.

Post a Comment

0 Comments