Mwalimu wa Singida Fountain Gate Ernst Middendorp amemtaja Gadiel kama mchezaji bora wa mechi kwa upande wake leo. Anasema katimiza majukumu yake kwa asilimia 100.
Lazima tukubaliane naye kwasababu yeye ndiye anayejua alimpa maelekezo gani siku ya leo.
Hapa mwalimu bila shaka ameanza kumtengeneza Gadiel anayemtaka.
Muda mwingine waalimu hawaangalii mchezaji atakuvutia vipi machoni kwa sanaa yake ya uchezaji, bali wanaangalia mchezaji gani atanipa nini kwa faida ya timu. Leo hii Gadiel Michael alikuwa mchezaji bora kwenye mbinu ya mwalimu lakini kwenye macho yetu inawezekana tukawa na mitazamo tofauti kwasababu tunapenda sanaa fulani tuione.
Je, tunakubaliana na mwalimu Ernst Middendorp???...
Je, unaweza ukawa mwendelezo wa Gadiel Michael kucheza kwenye kiungo???
Je, tunaweza tukayaona yale ya Kimmich ndani ya Gadiel??...
Majibu anayo mwalimu na atatujibu kwa muda
✍️ mlelwa_fred
0 Comments