Hot Posts

6/recent/ticker-posts

KELVIN KIJILI ELECTRIC⚡




✍️ Binafsi natamani kumuuliza Kelvin Kijili ni mchezaji gani anapenda kumuangalia zaidi??. Ni mlinzi gani wa pembeni barani Ulaya anapenda zaidi kuangalia video clips zake??.. Au ni fullback gani ambaye kwake Kijili ni favorite na mfano kwake??
 
✍️ Sijui majibu ya Kijili yatakuwaje lakini kama mimi ningepewa nafasi ya kumjibia maswali hayo, ningemtaja Kyle Walker wa Manchester City na timu ya taifa ya Uingereza. Inawezekana Kijili kwake ni tofauti lakini binafsi nauona Uwalker flani ndani yake. 
Huyu jamaa ana tembea sana kule pembeni sio masiala. 

✍️ Huyu ni aina ya wale fullbacks wanaowafungisha tela winga na fullback wake. Ni kama anawaambia kuwa nifuateni kama mnaweza.
Nimemfuatilia kwa ukaribu tangu amejiunga na Singida, Kelvin Kijili ni mafia kule pembeni. Anatembea sana kule kwenye touchline. Energy ileile dakika ya kwanza mpaka ya mwisho. 
 
✍️ Hajatengenezwa pale Asec wala Vita, ni mwenzetu kabisa huyu. Kijana wa ardhi hii hii ya Mwalimu Nyerere wa Butiama anakiwasha sana kwenye stage kubwa zaidi ya soka la Bongo kwenye level ya klabu. 
Kwasasa siyo mmoja kati ya mafullback bora nchini, bali ni mmoja kati ya wachezaji bora kabisa nchini.



✍️ mlelwa_fred

 

Post a Comment

0 Comments