Hot Posts

6/recent/ticker-posts

SPURS KIDOGO SANA WAIBONDE ARSENAL


✍🏻Mpira unaona unabondwa , unaona timu mbili ambazo zinafundishwa boli 

✍🏻Kitu ambacho Spurs walikuwa wanakabiliana nacho vizuri ni ile pressing ya Arsenal hasa ule mstari wa kwanza wa ulinzi wa Arsenal ( Saka Odegaard Nketia na Jesus ) walikuwa wanaishinda vizuri tu 

1: Muundo wao Spurs wa 2-3 wakiwa na mali ( Romero na VDV nyuma ) na mbele yao mstari wa wachezaji watatu Porro Bissouma na Udogie huku Maddsion akiwa kwenye namba 10 na Sarr anabadilisha nafasi kulia na ndani kwenye namba 8 

2: Kilicho wakwamisha Spurs baada ya kuishinda press ya Arsenal ni ile phase ya pili , ambapo mchezaji mwenye mpira ( mara nyingi akiwa Bissouma ) anakosa options za kutosha mbele yake kupasia mpira ... kwanini ? 

3: Kwasababu Arsenal walikuwa wanaweka presha kwenye mpira na mchezaji haraka sana ili kuwalazimisha Spurs kufanya maamuzi ya haraka ambayo sio sahihi 

✍🏻Nafikiri Arsenal kuna nyakati ambazo walikuwa katika ubora wao kama dakika 15-20 fulani . Walikuwa sharp sana , mpira unatembea haraka sana , movements nzuri sana kwa wachezaji wanaoshambulia space ilibaki kutoa adhabu kali . 

1: Nafikiri baadhi ya nyakati , Arsenal walikuwa wanaharakisha sana pasi kwenda mbele ( Verticatility ) badala ya kuongeza pasi zaidi ( Extra pass ) ili kudumisha umiliki wa mpira na sio kuutupa tena 

2: Mara nyingi hatari ya Arsenal inakuwa upande wao wa kulia ( White Odegaard na Saka ) lakini hakukuwa na quality kubwa leo hasa baada ya kutoka kwa Rice , kwanini ? Kwasababu Rice huwa anawapa option ya kukimbia mbele haraka bila mpira maana yake inachukua mawazo ya wapinzani kumfuata yeye na space kufunguka kwa Ode na Saka 

NOTE 

1: Napenda sana jinsi wachezaji wa Spurs wanavyobadilishana nafasi uwanjani bila kuharibu muundo wa timu yao wa 2-3-2-3 ni wachezaji wawili tu ambao hawabadilishi nafasi ( Romero na VDV ) 

2: Saliba kwenye mpambano wa 1v1 yupo vizuri sana 🔥

3. VDV akiwa na mali mguuni ✅ kwenye kuzuia ✅

4: Saka alikuwa anampika sana Udogie nashangaa kwanini hakupewa mipira mingi sana kutoa adhabu zaidi 

5: Maddison 🔥 Pauni Milioni 40 tu 

6: Jorginho kasinzia na kaadhibiwa 

7: YVES BISSOUMA anacheza kama hataki vile 🔥

FT: Arsenal 2-2 Spurs

 

Post a Comment

0 Comments