Hot Posts

6/recent/ticker-posts

MAKAME AJIWEKA TAYARI KWA DIRISHA DOGO LA USAJILI



Kiungo Abdulaziz Makame ‘Bui’, baada ya kukosa timu ya kuichezea anapigia mahesabu usajili wa dirisha dogo, huku akieleza anavyotakiwa kujitoa kuhakikisha analinda kiwango chake.

Makame aliyewahi kuichezea Yanga, Namungo na Kagera Sugar alisema kuna wakati anatafuta makocha wanaomsaidia kumnoa kiwango chake, wakati mwingine anajichanganya na mechi za mtaani, ili mradi kiwango chake kisishuke, ili akirejea kazini asianze upya.

“Siwezi kusema kwasababu nipo nje ya majukumu basi najiachia, najitambua na najua nataka nini kwenye soka, ingawa si rahisi inahitaji kujitoa kwani hakuna mtu anayekulazimisha kufanya mazoezi tofauti na inavyokuwa kwenye timu,” amesema na kuongeza;

“Zipo sababu nyingi za kukosa timu, wakati mwingine yanakuwa maslahi, ingawa siwezi kueleza kila kitu, kikubwa najipanga kwa ajili ya wakati mwingine, kazi yangu ni soka na bado nina umri wa kucheza mpira na kila hatua kwangu ni funzo,”.

Jambo jingine analolizingatia kwa kipindi hiki ni kuzifuatilia ligi mbalimbali, kuona ushindani ulivyo. “Naangalia Ligi Kuu ya Zanzibar, Bara na ligi za nje kwa ajili ya kujifunza vitu vingi vitakavyonisaidia kuvifanya nitakapopata timu ya kuchezea.”



 

Post a Comment

0 Comments