Kama mzazi wa mapacha wawili Kulwa na Dotto nimepata shida sana kufanya maamuzi kuwa sehemu ya shughuli mojawapo ya hawa vijana wangu vipenzi,kibaya zaidi shughuli zao zote zinafanyika nje ya nyumbani tena kwa wakati mmoja, shughuli ya Dotto ipo Ndola, Zambia na ya Kulwa ipo Kigali,Rwanda.
Kama mzazi nimeamua kubaki nyumbani ili kukwepa lawama kutoka kwa vijana wangu maana kila mmoja angependa niwe sehemu ya shughuli yake,nimeamua kuwaagiza baba zao wadogo nassibmkomwa_ aniwakilishe kwenye shughuli ya Dotto kule Zambia na mkazuzutza aniwakilishe kwenye shughuli ya Kulwa kule Rwanda.
Mimi nimebaki nyumbani Tanzania, sina cha zaidi ya kuwaombea vijana wangu wote wawili hii leo wapate matokeo kwenye shughuli zao huko ughaibuni.
Nawatakia kila la kheri wanangu Kulwa na Dotto na Mwenyezi Mungu akawasimamie leo mpate USHINDI mrejee nyumbani mkiwa na furaha tele.
0 Comments