Hot Posts

6/recent/ticker-posts

SASA NI RASMI YANGA VS EL MERREIK KUCHEZWA NCHINI RWANDA

Mchezo kati ya El Merreikh ya Sudan dhidi ya Yanga sasa rasmi utapigwa Uwanja wa Pele nchini Rwanda.


Awali El Merreikh ilikuwa na hesabu za kuuhamisha mchezo huo kuupeleka nchini Morocco lakini inaelezwa walishindwa kupata visa kwa wakati kuwahi muda wa kikanuni wa kubadilisha uwanja.


Yanga imethibitisha kwamba mchezo wao wa kwanza ugenini dhidi ya El Merreikh utapigwa Septemba 16, 2023 katika Uwanja wa Pele nchini Rwanda ambao awali ulijulikana kama Uwanja wa Nyamirambo.


Uwanja huo ambao umefanyiwa ukarabati mkubwa hauna kumbukumbu nzuri kwa Yanga kwani mara ya mwisho walipogusa hapo walipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao Rayon Sport mwaka Agosti 29,2018.


Matokeo hayo yaliwatupa Yanga nje na kuipa nafasi Rayon kutinga makundi ya Kombe la Shirikisho wakati huo ikifundishwa na kocha Roberto Oliveira 'Robertinho' ambaye sasa yuko Simba.



 

Post a Comment

0 Comments