Ni rahisi sana Rais wa Real Madrid kumwona Valdebebas mazoezini kila siku akiwa free, huwa anasema Urais sio kukaa ofisini na kama nina majukumu mengi basi hakuna jukumu kuzidi Real Madrid, Perez anauishi mpira na muda wote anataka kuwa na Wachezaji wake mpaka photoshoot za msimu na hafla za Christmas Mzee anataka kuwepo na huwa anawepo.
2016 hii kwenye hotel ya Royal Peak nchini Japan ndio inatajwa Rais alitumia muda mrefu zaidi kupiga picha na Mashabiki, kusaini jezi zao na kupiga nao stori! Rais anasema yeye anaongoza Real Madrid na hao ndio Maboss zake, hataki Shabiki ahisi ni ndoto kukutana nae kwakuwa maisha ya mpira ni tofauti na taasisi nyingine, Perez anajichanganya saana ndio approach ambayo yeye anaona ni sahihi kuliko kujifungia tu ndani.
Kupitia kujichanganya huku ndipo alimpata Mchezaji Marco Asensio kwenye visiwa vya Mallorca alipoenda tu kula bata (Nitawapa kisa hiki) huku kwetu nafurahi kumwona Mhandisi mwingine caamil_88 akiishi utamaduni huu, utamaduni wa kisasa wa Rais kuwa karibu na Wachezaji na Mashabiki, wafuatilie Viongozi wengi wa muundo huu hakuna aliyefeli, Abramovich, Nasser, Agnelli na wengine! The new era has began.
VISIT MOROGORO🇹🇿
0 Comments