Hot Posts

6/recent/ticker-posts

SIMBA HAITAFUZU MAKUNDI MALISA AWAJIBU WANAOISEMA VIBAYA SIMBA


Wacha-MBUZI uchwara wameanza kupiga ramli kama kawaida yao. Kwa mtu yeyote anayejua mpira hana wasiwasi na Simba kwenda group stage. Ni kweli jana tumecheza chini ya kiwango, tumefungwa magoli ya "kindezi" lakini sio justification ya kushindwa kwenda makundi. Makosa mengi tuliyofanya uwanjani jana ni makosa yanayoepukika. Kwahiyo msianze kubet mechi ijayo. Mtaliwa vibaya, nawahurumiaa (kwa sauti ya Mchungaji Magembe) 🤣🤣.

Mnakumbuka mlipiga ramli hivihivi tulipocheza na Horoya? Kule kwao Guinea wakatupiga 1-0. Wacha-MBUZI wakasema safari yetu imefika mwisho. Lakini walipokuja Lupaso nini kilitokea?

Tuliwapa HAKI YAO YA KIKATIBA na tukahakikisha tunawaingiza kwenye vitabu vya kumbukumbu za CAF. Tuliwapiga kama tunaua kiboboru. Kile kipigo hakijawahi kutokea ukanda wote wa Afrika mashariki kwenye mashindano ya CAF. Tuliwapiga mpaka wakasema Mbowe sio gaidi. Kipigo cha 7-0 kiliwafanya wakiri imani ya mitume na kusoma waraka wa kwanza wa Paulo kwa Wafilipi.

Wacha-MBUZI walewale waliotusema vibaya mwanzoni wakabadili gear angani fasta, na kusifia kipigo hicho cha kihistoria. Kwahiyo nashauri wacha-MBUZI waache kupiga ramli. Wajikite kwenye mechi ya jana. Waeleza mapungufu yaliyojitokeza jana yakaigharimu Simba. Waeleze kuhusu kipa, ubutu kwenye safu ya ushambuliaji, Kocha kushindwa kupangilia kikosi etc. Waache kuchambua mechi ambayo haijachezwa bado.

Eti Simba hatuingii makundi?? Mtakua mnaumwa kifaduro si bure. Makundi pekee ambayo tunaweza tusiingie ni ya michango ya harusi na VICOBA. Lakini makundi ya klabu bingwa Afrika, tunaingia na miguu, mikono, ndevu, kucha na mawigi. Kwa kifupi tunaingia mwili mzima. Bata, Wahed.!

 

Post a Comment

0 Comments