Kocha Mkuu ya Klabu ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Mfaransa Julien Chevaliar aliyekuwa anamfundisha kiungo Pacome Zouzoua akiwa kwenye timu hiyo ya Ivory Coast, amesema alichokionesha Pacome Yanga SC mpaka sasa ni asilimia 40 ya kiwango chake halisi na kuwataka washabiki wa Yanga watarajie makubwa.
Pia kocha huyo amesema aliumizwa mchezaji huyo alivyoondoka klabuni hapo
“Namkumbuka sana Zouzoua, ni kijana wangu, watu hawajui hiyo timu iliyomsajili (Yanga) ilipomchukua Aziz Ki wakati ule,tulimchukua Zouzoua kuziba nafasi yake na msimu wa kwanza alituonesha kwa nini tulimuamini,niliumia sana alipokuja kuniaga kuja huko (Yanga)” —
Amesema Chevalier akizungumza na Gazeti la Mwanaspoti.
0 Comments