Inapendeza kuona namna flani timu hii inapambana kujitegemea, kwa mara ya kwanza ilifanyika SIMBA DAY msimu huu bila fedha kutoka mifuko ya watu bali Wadhamini wa klabu na vyanzo vingine vya mapato, inapendeza kuona hatua kwa hatua timu inaanza kuondoka kwenye minyororo ya utegemezi kwa 100% ni hatua nzuri kuelekea nchi ya ahadi.
Mashabiki wa Simba ongezeni kasi ya kudownload App ya SIMBA APP, ongezeni kusubscribe Youtube mkatengeneze numbers, hii ina maana kubwa kwa maslahi ya klabu! Changamoto ni Maudhui kuwa madogo, ubunifu na vifaa, nadhani CEO twist kidogo wekeza tu kwakuwa Vijana walioaminiwa wapo vizuri changamoto ni vifaa.
YANGA wameanza kutengeneza namba kupitia Youtube, ni wake up call! Mashabiki tupunguze stori nyingi, tufanye jezi bei, tufanye tiketi bei! Basi hata BUKU MBILI ya APP? Au MB kadhaa za Youtube ya SIMBA? Tupunguze stori stori na siasa nyingi, dunia ni digital! Shida kubwa ya Mashabiki wa Simba tukiambizana ukweli utasikia UNATUMIKA, UNATUGOMBANISHA.
Leo hii namba zinatuhukumu haswa Youtube, lets get it done! Tupunguze stori! Tuingizie pesa klabu, kama una smart download App na nenda Youtube, na kitengo cha Kaka @ahmedally_ zidisheni maudhui zaidi, tuwe na ukubwa kila eneo kuliko kuvimbia huku na namba tunapigwa baadhi ya maeneo, LETS MAKE IT POSSIBLE.
Target yetu, revenue za Youtube, renevue za APP, huku Instagram na Twitter hakuna hela zaidi ni informations tu! Sina shaka na uwezo wa HOMEBOY @thobias17sebastian sina shaka na uwezo wa @babchicharito2407 Au Shemeji @rabbihume issue ni INVESTMENT HATUNA👊
Bado hatujaweza faidika na fanbase kubwa ya Simba mtandaoni, kuna mawili mwamko mdogo ama maudhui hakuna, tusolve vyote kwa pamoja.
0 Comments