Beki wa kimataifa wa Tanzania Abdallah Shaibu 'Ninja' ameanza mechi yake ya kwanza katika timu yake ya Lumbumbashi Sport akicheza Kwa dakika 90 na kuonekana kukubalika na mashabiki waliokuwa wakimpongeza baada ya mechi.
Ninja aliyeachana na Yanga msimu uliopita aliichezea timu yake hiyo dhidi ya klabu ya Don Bosco na kumalizika Kwa 1-1 huku Ninja akionesha kiwango kizuri.
Baada ya mechi hiyo mashabiki walimpigia makofi na wengine waliopata bahati ya kuwa naye karibu walimpongeza Kwa kazi nzuri japo ndio ilikuwa mara ya kwanza kucheza tangu ajiunge na timu hiyo.
0 Comments