🗣️Tatizo kubwa kwa mashabiki wa soka hapa Tanzania na viogozi kwenye klabu kongwe wanapenda kuthamini na kuwapa sifa kubwa wachezaji wa kigeni bila kujali uwezo wao na kuacha kuwapa vipaombele wachezaji wazawa wenye viwango bora
🗣️Mzamiru yassin msimu uliopita ndiye kiungo aliyekuwa roho ya timu na kuifanya timu kuwa na ubora katika mechi nyingi kuanzia za ndani na kimataifa, Lakini ujio wa Fabrice Ngoma ndani klabu ya Simba watu wanataka kulazimisha kwa Ngoma anauwezo mkubwa wa kumzidi Mzamiru, Mbaya zaidi wanatamani Fabrice Ngoma apate nafasi ya kucheza kuliko Mzamiru yassin ambae amekuwa bora katika vipindi vyote ndani ya klabu ya Simba
🗣️ Mzamiru ndiye kiungo bora wa kati kwasasa ndani ya klabu ya Simba, Hakuna kiungo wakumfikia na Anastahili kupata mshaara mnono kuliko kiungo yeyote ndani ya klabu ya Simba kutokana na ubora wake na mchango anaoutoa na kujituma kwake ndani ya kikosi
0 Comments