Kwa misimu ya hivi karibuni hatupo vizuri kitu ambacho kilipelekea msimu uliopita watu kutishiana kusomeana albadili kutokana na baadhi kuhisi kuwa kuna wasaliti ndani ya timu.
Msimu huu wazee wetu kuanzia Lushoto, Handeni, Muheza na maeneo mengine yote ya Tanga wamesema hapana, tukae tuangalie nini tatizo na sasa hivi Tanga yote imekuwa moja na watu wamekula viapo safari hii tunakwenda na Coastal Union.
Na katika viapo hivyo wazee wetu wameanza kwa kutafuta fedha, wamemleta mdhamini mkuu ambaye juzi tumemtangaza na amesema hataki kuwa kwenye timu ambayo itakuwa kwenye presha ya kushuka daraja au ipo kwa ajili ya kushiriki Ligi.
Mdhamini mkuu anataka aione Coastal Union ikimaliza katika nafasi nne za juu ili kupata nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa na yeye apate kujitangaza kimataifa.
- Abbas El-Sabri, Ofisa Habari Coastal Union.
0 Comments