Tayari ubora umeanza kuleta ushindani mkubwa na mwishoni mwa msimu kutakuwa na majibu sahihi.
Kapombe wa Simba amekuwa mfalme wa nafasi hiyo kwa muda sasa lakini misimu miwili ubora wa Djuma Shabani ukawa ni ushindani mkubwa na wakati mwingine kuwagawanya, kila mmoja akiamini tofauti.
Sasa kuna kuna Yao wa Yanga, naye ameonyesha kazi ipo na uwezo upo. Hata kama ni mwanzo lakini kazi imeonekana.
Usimsahau Lusajo kutoka Azam FC ambaye kwenye ubora wa ulinzi na kusaidia mashambulizi amekuwa bora.
Bila shaka ni lazima tuupe muda ushindani huu kuanzia Simba, Yanga, Azam, Singida na timu nyingine...lazima jibu LITAPATIKANA TU.
0 Comments