Hot Posts

6/recent/ticker-posts

SAFARI YA NOVATUS DISMAS ANAYECHEZA UEFA ULAYA NI MATUMAINI KWA VIJANA WENGINE TANZANIA


Safari huwa na mambo mengi sana na njiani uvumilivu unahitajika.


Taarifa za Novatus Dismas sasa kwenda Shakhtary Donesk, timu inayoshiriki Uefa Champions League ikiwa kundi moja na FC Barcelona ni habari kama sherehe ya taifa ya mpira wa miguu.


Wako walianzisha njia lakini tulikuwa kama tumekwama hivi lakini Dismas anakuwa kijana mwingine ambaye ameamsha matumaini 2023 kuwa INAWEZEKANA.


Azam FC, Alliance wanastahili PONGEZI KUBWA SANA kwa malezi ya huyu kijana lakini kote alikopita kama Biashara united ambao walimsaidia kupata uzoefu.


Safari yake ya Israel, Ubeligiji na sasa mwanga umewaka lazima wako wanamsimamia na kumuongoza...tuwapongeze.


Mwisho niwasisitize vijana wengine wakae chini waichore njia aliyopita Dismas na kuanza kujifunza, hata kama kila mmoja ana njia yake lakini kuna njia inaweza KUFANANA
 

Post a Comment

0 Comments