WHAT A GAME .!!!
✍🏻Kama umekosa hii mechi daah , umekosa burudani sana mpira mwingi sana umepigika , Bayern Munich Vs Bayer Leverkusen
✍🏻Dakika kama 10 za mwanzo , Bayern walitumia nafasi nzuri baada ya Leverkusen kusita kwenda kukabia juu maana yake Bayern wakawa na watu wengi zaidi ya Leverkusen kwenye build up ( creating overloads )
1: Bayern walikuwa na watu 5v3 dhidi ya Leverkusen
2: Kwenye muundo wao wa 2-3 ( Upamecano na Kim nyuma ) huku mbele yao mstari wa Laimer Kimmich na Davies
3: Leverkusen walikuwa wanazuia kuanzia juu na watu watatu ( Hoffman Boniface na Wirtz ) maana yake Bayern walikuwa wanatoka vizuri nyuma
✍🏻Pale tu Leverkusen wingbacks wao ( Grimaldo na Frimpong ) walipoamua kusogea juu kusaidia pressing ndipo Leverkusen walipoingia mchezoni maana yake Frimpong na Grimaldo walikuwa wanawazuia vizuri Davies na Laimer , faida yake ?
1: Bayern walikosa njia ya kutoka ( Outball ) ambao walikuwa ni fullbacks wao
2: Iliwapa nafasi Xhaka na Andrich kuwa press zaidi Kimmich na Goretkza , hapo kuwalazimisha Bayern kupiga mipira mirefu ambayo ni rahisi kwa mabeki watatu wa nyuma ya Leverkusen kukabiliana nayo
✍🏻Kuna nyakati Bayern walikubali kuingia mtego wa Leverkusen ( Baiting the press ) yani Leverkusen kama wanataka Bayern wawafanyie press ili space ifunguke nyuma ya kiungo cha Bayern na walifanikiwa maana Florian Wirtz alikuwa anapata space kubwa sana nyuma ya kiungo cha Bayern . Shida ni : Leverkusen hawakushambulia na idadi kubwa ya wachezaji
✍🏻Kipindi cha pili , rusha shilingi yako juu ... yoyote angeweza kushinda mechi kutokana na idadi ya nafasi nzuri ambazo timu zote zilipika na umaliziaji ulikosekana au niseme tu Makipa walikuwa hodari .
NOTE
1: Leroy Sane kwenye ubora wake leo hatari sana 🔥
2: Ile Freekick ya Grimaldo 🔥
3: Xhaka kama hataki vile kwenye kiungo , anaachia tu mali hataki kukaa nayo
4: King Kane hata Bundesliga anafunga tu
5: Florian Wirtz alifanya kila kitu sahihi kuna nyakati pasi za mwisho zilimuangusha
5: Ukiacha mara moja tu kila mmoja alipikwa lakini mechi kwa kiasi kikubwa walicheza vizuri sana : Tapsoba na Kossounou 🔥🔥
FT: Bayern 2-2 Leverkusen
0 Comments