Hot Posts

6/recent/ticker-posts

SIMBA SISI HATUGAWANYIKI


 Baada ya Yanga kukaa kileleni mwa NBC Premier League na washabiki wao kuendelea na tambo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC,Salim Abdallah “Try Again” amesema kelele hizo haziwatoi mchezoni na malengo yao ya kubeba makombe yote nchini yapo palepale, wakiwa tayari washaanza la ngao ya Jamii. 


"Kama kikosi tunajivunia kuanza vyema msimu huu kwa kufanikiwa kushinda taji la Ngao ya Jamii na dhamira yetu ya kuendelea kukusanya makombe inaendelea”


"Kumekuwa na kelele nyingi za mashabiki wa timu mbalimbali,lakini kwetu malengo makuu ni mataji na hesabu zetu ni kushinda makombe yote, hivyo kelele hazitutoi mchezoni” Amesema Try Again kupitia gazeti la Champion.

Post a Comment

0 Comments