Baada ya kusoma comments za wadau imebidi nirudi tena kutetea point yangu.
Naona kuna mjadala unaendelea mtandaoni eti "kila kocha ana Falsafa yake"
Ni kweli kila kocha duniani ana Falsafa yake mfano Klopp ni muumini wa "Heavy metal football" Pep guardiola ni muumini wa "Total football" Jose Mourinho ni muumini wa "Hit or lose" Diego Simeone ni muumini wa kupaki bus na kupiga Counter-attack"
Yes! Kila mtu ana style yake ya uchezaji (style of playing) lakini hizo style zote ili zifanye kazi intensity kwa wachezaji inahitajika.
Mfano Diego Simeone,anapaki basi kisha wapinzani wakisogea kwenye zone yake wachezaji wake watatakiwa ku-press kwa intensity ili kuiba mpira na kuanzisha Counter-attack.
Pep Guardiola timu yake inapiga pasi nyingi lakini ikipoteza mpira ina-press kwa Intensity.....hivyo intensity ni kitu muhimu kwenye kila aina ya uchezaji.
Intensity inatengenezwa kwenye uwanja wa mazoezi....unahitaji wachezaji wako wawe fit kimwili na kiakili ili kucheza kwa Intensity.
Mimi sizungumzii "Falsafa" nazungumzia ukosefu wa Intensity kwenye uchezaji wa Simba.
Tatizo la Simba msimu huu wana wachezaji baadhi ambao fitness yao iko chini....mfano Sadio Kanoute,Saido Ntibazonkiza,Onana,Miquisson etc..
Kanoute ni mtu muhimu kwenye pressing ya Simba lakini msimu huu hayuko sawa....Saido haonekani kuwa na Sharpness akiwa na mpira na bila mpira....Onana the same.
Hivyo sasa hivi ni Rahisi wapinzani kufika kwenye lango la Simba bila usumbufu wowote....tazama jana Coastal Union wamekosa nafasi ngapi?
Tunazungumza haya yote kwasababu Simba italiwakilisha taifa kwenye michuano ya kimataifa hivyo tunawatakia mema....Robertinho na Fitness Coach wake bado wana kazi ya kufanya.
Huu ujumbe watauelewa watu wanaojua mpira lakini ukileta ushabiki huwezi kuelewa.
0 Comments