Hot Posts

6/recent/ticker-posts

KUMBE WAZIRI WA MICHEZO DAMAS NDUMBARO ALIFUNGIWA NA TFF?? SASA ITAKUWAJE TFF WATOA MAJIBU


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linapenda kutoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa zinazoenea mitandaoni kuhusu kufungiwa kwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro. 
Usahihi ni kuwa Waziri Dk Ndumbaro alifungiwa miaka saba na uongozi uliopita wa TFF. 

Hata hivyo, hakukubaliana na uamuzi huo ambapo alikata rufani katika Kamati ya Rufani ya Nidhamu ya TFF kupinga adhabu hiyo. 

Hivyo, Kamati ya Rufani ya Nidhamu ya TFF chini ya uongozi wa sasa ilisikiliza rufani hiyo mwaka 2017 ambapo Waziri Dk Ndumbaro alishinda, hivyo kuondolewa adhabu ya kufungiwa. 




 

Post a Comment

0 Comments