🚨 KIVUMBI. Kama hujui leo kuanzia saa 2:00 usiku kitaeleweka barani Afrika wakati droo ya michuano mipya ya Ligi ya Afrika (The Africa Football League, zamani CAF Super League) itakapofanyika na Simba itajua itaanza na nani katika michuano hiyo itakayoshirikisha VIGOGO nane tu.
.
Droo hiyo itafanyika makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Cairo Misri na SIMBA ndio wawakilishi pekee wa Tanzania 🇹🇿 na Ukanda wa Nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) waliopenya michuano hiyo itakayoanza rasmi mwezi ujao ikiwa hatua ya robo fainali.
.
VIGOGO wengine watakaoshiriki leo kusikilizia droo hiyo ni; Al Ahly (Misri), Esperance (Tunisia), Wydad Casablanca (Morocco), Enyimba (Nigeria), TP Mazembe (DR Congo), Petro de Luanda (Angola) na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
.
Michuano hiyo itazinduliwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Oktoba 20 na siku hiyo ndipo SIMBA itacheza mechi ya kwanza nyumbani dhidi ya mpinzani atakayejulikana leo na baada ya hapo mechi zitapigwa kwa muda wa wiki nne na kutamatika katikati ya Novemba.
0 Comments