Hot Posts

6/recent/ticker-posts

HAKUNA NJIA YA MKATO KWA AZAM FC



Timu ya soka ya Azam FC inakomazwa, kichapo ilichopokea hivi karibuni kutoka Kwa Bahir Dar Kenema ya Ethiopia na kutupwa nje ya mashindano ya kombe la shirikisho barani Afrika ni sawa na vipigo kama hivyo ambavyo Yanga na Simba zimewahi kukumbana navyo hadi kufikia hapa zilipo.

Simba imetawala soka la Tanzania miaka ya hivi karibuni na kushiriki mara kadhaa mashindano ya Ligi ya mabingwa Afrika lakini ni baada ya uwekezaji mkubwa na usajili bora na kufungwa na timu bora mara kadhaa.

Mashabiki wanapotazama usajili wa Azam na maandalizi iliyofanya kuelekea mashindano ya kombe la shirikisho, wanafanya kosa kwani haraka wanaiweka katika mezani moja na Yanga na Simba.

Pia mashabiki na hata wachambuzi wa soka wanapotazama baadhi ya nyota waliosajiliwa na miamba hiyo ya Chamazi, hawaoni sababu kwanini ishindwe wakati usajili wake ni karibu sawa na ule wa mabingwa wa soka nchini Yanga na hata Simba.

Kwa mtazamo wangu kitendo Cha Azam FC kuondolewa katika hatua ya awali ya kombe la shirikisho barani Afrika kinaijenga, kinaikomaza, kinasababisha uongozi upitie kasoro zilizopo na kufuata njia waliyopita Yanga msimu 2012/22.

Kilichowakuta Azam FC msimu huu ndicho kilichoitokea Yanga msimu wa 2021/22 katika mashindano ya Ligi ya mabingwa barani Afrika ilipoondolewa katika hatua za awali na Rivers United ya Nigeria baada ya kuchapwa michezo yote miwili yaani ndani na nje.

Matokeo hayo yalionekana kuwakatisha tamaa mashabiki wa klabu hiyo ya Jangwani kuelekea msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara huku wakiwa na kumbukumbu ya kukaa miaka minne bila taji. Katika kipindi hicho utawala wa soka nchini ukiwa chini ya miamba ya Msimbazi ambayo ilikuwa inafanya vizuri ndani na nje.

Kabla ya kuanza Kwa msimu wa 2021/22 Yanga ilifanya maingizo mapya ya wachezaji kutoka ndani na nje ya nchi wakiwa na uzoefu wa kutosha kama ilivyo Kwa Azam FC msimu huu. Matarajio yao yalikuwa kufanya vizuri katika mashindano ya klabu Afrika na ligi kuu Tanzania Bara.

ITAENDELEA................

@azamfcofficial @hasheem_ibwe @zakazakazi

 

Post a Comment

0 Comments