Kocha wa Singida Fountain Gate, Ernst Middendorp kupitia mahojiano aliyofanya na kituo cha Habari cha 947 Joburg kutoka Afrika Kusini amezungumza mengi lakini machache kati yake ni kuwa aliona kuwa katika siku za baadaye uongozi wa Singida ungeingilia majukumu yake na kuanza kumpangia wachezaji anaotakiwa kuwatumia kwenye mechi.
“Sijali wengine wanafikiria nini nataka kufanya kazi kama kocha na najua ni nini nafanya, napokea message nyingi kutoka kwa wachezaji na hii inaonyesha kujali na ninajivunia hilo.
“Niliona huko baadaye nitakuja kuambiwa sio golikipa huyu mchezeshe huyu, sio beki huyu mchezeshe mwingine, sio hawa viungo wawili wachezeshe hawa wawili hiki ni kitu ambacho nilikiona kitakuja kutokea baadaye na hiyo haifanyiki kwangu, mimi siwezi.
“Waziri wa Fedha, Mmiliki wa Klabu, Mwenyekiti wa Klabu na Menejimenti wote hawapo kwenye uwanja wa mazoezi, hawaoni wachezaji wakifanya kazi hawaoni wachezaji wakimudu mchezo, hawana idea ni Mchezaji gani amejiandaa vizuri kwaajili ya mchezo,”.
0 Comments