Hot Posts

6/recent/ticker-posts

KUMZUIA YANGA NI KUJIPA TABU MSIKIE GAMOND ….


Namungo wamejitahidi sana kuzuia kwa nidhamu kubwa, tena kubwa sana. Waliujua ubora wa Yanga katikati nao wakaweka idadi kubwa ya viungo ili kutowapa mwanya katikati.


Na kwa bahati mbaya kwa Yanga, kabla ya Moloko kuingia hakukuwa na mtu anayependa kucheza kwenye mstari. Hakuwepo atakayetanua uwanja kuitafuta nafasi kubwa pembeni. Hii ni kwasababu Aziz Ki, Pacome na Max wote wanapenda kucheza katikati kwahiyo wanabadilishana sana nafasi.


Gamondi alirudi kwenye mkoba wake wa mbinu na kumleta Moloko ambaye alikuja kuwa na faida sana kwenye namna Yanga wanavyoshambulia.


Ingekuwa alama moja kubwa sana kwa Namungo kwa jasho walilomwaga lakini haijawa. Ndiyo football 


Aliyekuwa bora ameshinda....


✍️ @mlelwa_fred 

Post a Comment

0 Comments