Hot Posts

6/recent/ticker-posts

MIDDENDORP NA SURA HALISI YA KIJERUMANI😊😁🙌



Umeshtushwa na taarifa inayozagaa mitandaoni kuwa kocha Ernest Middendorp ameamua kuikacha Singida? 

Kama umeshtuka nikuambie tu hakuna maajabu! Wakati tunasubiri taarifa Rasmi ya klabu nikuambie Kocha huyu ni wa hivyo! Haogopi kufanya maamuzi magumu.

Kwake Nyeusi sio dark blue😊 Ukisema ni nyeusi kwake mtaelewana ila usimwambie ni nyeusi kwa umbaaali... Ataondoka tu.

Alishawahi kuwapelekesha puta Orlando Pirates mpaka wakajuta kumpa mkataba 😁 Yeye haogopi kuwaambia ukweli wenu mnapoenda tofauti na mabegi yake haoni shida kubeba!

Maritzbug nao walionja joto lake! Ni mwalimu mwenye msimamo wa KIJERUMANI na ni bonge la Kocha ukimtimizia mahitaji yake! 

Kanyooka kama msonobari Baba yule! 
Kama walikuwa wanafanya kazi kwa kumpangia kazi kama mitandao inavyodai basi Tusubiri barua yenye kichwa TUMEPOKEA KUJIUZULU au MAKUBALIANO YA PANDE ZOTE MBILI😁

Sema kafanya haraka kama anafunga Nyama robo😁


Post a Comment

0 Comments