Nguli wa soka, Cristiano Ronaldo amesema yeye na Lionel Messi wamefanikiwa kubadili historia ya mchezo wa soka, na kwamba upinzani baina yao kwa sasa umemalizika.
Wawili hao wanachukuliwa kuwa ni kati ya wachezaji bora wa soka kuwahi kutokea kwenye historia ya mchezo huo duniani, na walipambana vilivyo katika ligi ya Hispania kwenye timu za Barcelona na Real Madrid.
Ronaldo anasema kikubwa zaidi ni kwamba wanaheshimika duniani kote na kwamba Messi alifanya kwa uwezo wake na yeye alifanya kwa uwezo wake na wameweka heshima kwenye soka la kisasa.
Alipoulizwa kama kuna chuki baina yao, Ronaldo amesema haoni kama kuna kitu kama hicho na kwa wale wanaompenda yeye haikuwa na haja ya kumchukia Messi kwa sababu wote walikuwa kwenye ubora wa hali ya juu.
0 Comments