Huyu Mzee ametoa chozi ndani ya Makao Makuu ya Shirikisho la soka Afrika, nilikuwa namtazama kabla hawajatangaza Mshindi alikuwa hatulii kwenye siti, anageuka kulia na kushoto, mara mikono aweke kifuani mara shavuni, mara akae kwa kutazama tu, anafahamu nchi yake Tanzania ipo kwenye kundi la Simba wakali kama Algeria aliye tayari wakati wowote na Misri ambaye ndipo hapo walipo, anawaza bendera ya nchi yake, anawaza hatma za Mamillion ya Watanzania, ndivyo ilivyo wakati watu wapo kwenye mission kwa ajili ya nchi.
Wakati Patrice Motsepe anaitaja Afrika Mashariki, huyu Mzee alishindwa kusimama, alishindwa kupiga makofi akaamua tu kulia wakati huo Watanzania wengine na Wana Afrika Mashariki wanashangilia, kutoka Tanga mpaka Karume, hata kama Karia hatokuwepo basi wakati mnalifukia jeneza lake mkumbuke alilipigania taifa lake, machozi yanatoka kwakuwa hii ndio Tanzania yake, nyumbani kwake na hana kwingine.
Ujumbe kwa kizazi cha kesho, msiache ile video ipotee ya kuwa Mwanaume mmoja alilia kwa ajili ya taifa lake!
📸 eliabennet
VISIT TANZANIA🇹🇿
0 Comments