Hot Posts

6/recent/ticker-posts

KOCHA WA YANGA GAMONDI AMBADILISHA KILA KITU SKUDU


Kama wewe ni shabiki wa Yanga na ulikuwa unajiuliza kwanini winga kutoka Sauzi, Mahlatse ‘Skudu’ Makudubela hachezi licha ya kupona kutoka majeraha, basi kuna sapraizi mpya utakayokutana nayo, iwapo mchezaji huyo atapangwa kwenye pambano la marudiano la Ligi ya Mabingwa Afrika wikiendi hii.
.
Kama Skudu atapewa nafasi basi, mashabiki watakutana na sapraizi ya kipekee kutokana na kocha wa Yanga, Miguel Gamondi kumbadili karibu kila kitu. Skudu mpya ambaye ataanza kuonekana uwanjani hivi karibuni hana vionjo saana vya kuuchezea mpira na badala yake yuko tofauti akikamata mpira basi anaingia nao kutengeneza nafasi za mabao kama sio kukufunga hii ikiwa ni kazi iliyofanywa na kocha Gamondi aliyemtaka abadili aina ya uchezaji wake.
.
Gamondi amekuwa akizuia mambo mengi ya kuchezea mpira aliyokuwa akiyafanya Skudu akihofia wataendelea kumuumiza winga huyo ambaye anarejea kutoka majeruhi iliyomweka nje kwa muda kidogo.
.
Gamondi kwa sasa anataka Skudu akikamata mpira, basi akili iwe kuingia kwenye eneo la hatari la wapinzani au kutengeneza pasi au krosi za mabao kwa wenzake badala ya kuonyesha zile ‘shibobo ‘ alizozoeleka nazo.
.
Tayari Skudu ameshaanza kushika masharti hayo ya Gamondi akiwa na moto mkali akiwa mazoezini na sasa yuko tayari kuanza kuonekana kuanzia mchezo wa Septemba 30 Yanga itakapomalizana na Al Merreikh ya Sudan katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya mtoano.

 

Post a Comment

0 Comments