Hot Posts

6/recent/ticker-posts

HARRY KANE AFANYIWA FIGISU UJERUMANI


Harry Kane alifanikiwa kufunga magoli matatu katika mchezo mmoja kwa mara ya kwanza tangu kujiunga na Bayern baada ya kuondoka kwenye klabu yake ya utotoni, Tottenham Hotspur, wakati The Bavarians ilipoishushia kipigo kizito Vfl Bochum cha 7-0 katika mechi ya Bundesliga.

Kwa Nchini England na hata hapa Tanzania, magoli matatu katika mchezo mmoja kwa mchezaji huitwa 'hat-trick' na Kane alifikiri kwamba alikuwa amefunga hat-trick yake ya kwanza akiwa nchini Ujerumani, lakini kwa mujibu wa bizarre German rule, Kane kiufundi bado hajafunga hat-trick yake ya kwanza akiwa Bayern kwani Nchini Ujerumani, m/wachezaji lazima wafunge magoli yao matatu kwa utaratibu na kwenye kipindi kimoja cha mchezo bila ya mchezaji mwingine kufunga katikati ya kuisaka hat-trick.

Hii inamaanisha kuwa kwa sababu magoli ya Kane yalifungwa kati ya nusu zote mbili na wachezaji wengine wa Bayern wakifunga katikati yake, kiufundi bado hajafanikiwa kufunga hat-trick yake ya kwanza ya Bundesliga.

Mfano wa hili liliwahikutokea wakati wachezaji wawili wa Borussia Dortmund ambao kwa sasa wanacheza katika klabu mbili tofauti za Manchester, yaani Erling Haaland na Jadon Sancho.

Ambapo Haaland alifunga magoli matatu katika nusu ya pili ya mechi yake ya kwanza ya Bundesliga katika ushindi wa 5-3 dhidi ya Augsburg mwezi Januari 2020, lakini haikutambuliwa kama ni hat-trick kutokana na Sancho kufunga bao katikati ya goli la kwanza na la pili la Mnorway huyo.


Post a Comment

0 Comments