Hot Posts

6/recent/ticker-posts

KIWANGO CHA AZIZ KI CHINI YA GAMONDI NI BALAA!

 


🚨 Chini ya Kocha Nabi, Yanga ilikuwa na Feisal Salum ‘Fei Toto’ na Stephan Aziz Ki waliocheza namba 10 na wote walipata nafasi ya kucheza. Msimu huu Feitoto hayupo na Kocha Gamondi anamtumia zaidi Aziz Ki na Zouzoua Pacome na wakati mwingine Maxi Nzengeli kwenye kupandisha mashambulizi.

.

Vyovyote atakavyomtumia Aziz Ki, amekuwa na mchango mkubwa msimu huu na amefunga na kuchangia mabao msimu huu katika mechi sita za timu hiyo hadi sasa kabla ya mchezo wa jana dhidi ya JKT Tanzania. Ubora wa Ki unamsumbua kichwa Gamondi wa nani aanze kati yake Maxi na Pacome ingawa amekuwa akiwatumia wote kwani na amekuwa akifanya mzunguko kwenye kuchagua wachezaji na wote kufanya vyema. Ni namna tu atakavyowatumia.

Post a Comment

0 Comments