Hot Posts

6/recent/ticker-posts

CEDRICK KAZE BAADA YA KUTOKA YANGA AMEANZA KUSOTA NAMUNGO


CEDRICK Kaze alikuja nchini kwa mara ya kwanza akiwa kocha mkuu wa Yanga tukampa sifa kibao kutokana na wasifu wake katika ukocha. Aina yake ya soka ikapewa jina la Kazelona ikilenga kuonyesha kuwa imeambatana na maufundi ambayo alikuwa akiyatoa katika akademi ya Barcelona ambako ndiko alikokuwa akifanya kazi kabla ya kuja hapa.
.
Lakini Kazelona ikaelemewa na matokeo ya uwanjani na kupelekea kocha huyo wa mpira kupewa mkono wa kwaheri lakini baada ya miezi kadhaa akarudishwa nchini kuwa msaidizi wa Nasreddine Nabi. Mungu akawasikia bwana kwani timu ilifanya vizuri nje na ndani. Ikachukua Ngao ya Jamii, Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho la Azam na kisha ikaingia fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
.
Mafanikio yana gharama zake na ndio kilichotokea kwani Nabi aliamua kutoendelea kuitumikia Yanga, jambo lililofanya benchi lake la ufundi kuwekwa kando na uongozi wa timu hiyo kuamua kumpa nafasi kocha Miguel Gamondi. Nabi akatimkia zake FAR Rabat huku msaidizi wake Kaze akienda Namungo FC kuwa kocha mkuu, jambo ambalo wengi tuliona ni fursa muhimu kwa kocha huyo kuthibitisha kuwa anastahili kusimamia timu akiwa kocha mkuu na mafanikio yaliyopatikana Yanga akiwa msaidizi yalikuwa na mchango wake.
.
Hata hivyo, hajaanza vizuri ndani ya Namungo kwani katika mechi mbili za kwanza nyumbani dhidi ya JKT Tanzania na KMC amepata pointi moja tu. Ninachomsihi ni kwamba arekebishe mapema hali ya mambo kwenye timu ili irudi kwenye mstari na kututhibitishia kuwa wasiwasi ulioko juu yake kuwa hamudu kuwa kocha mkuu na kufanya vizuri hauna mashiko.



 

Post a Comment

0 Comments