Hot Posts

6/recent/ticker-posts

YANGA SC KIFALME KWENYE ARDHI YA NYUMBANI


Mpaka sasa Yanga SC imeshacheza jumla ya michezo minne na haijaruhusu hata bao mmoja ndani ya dakika 90


Yanga SC 2-0 Azam FC

Simba SC 0-0 Yanga SC

Asas 0-2 Yanga SC

Yanga SC 5-0 KMC FC


Waliondoka wachezaji kama Fiston Mayele, Yannick Bangala, Djuma Shaban, Benard Morrison na wengine wengi


Niliwahi kuandika hapa, Yanga SC ni Taasisi haimtegemei mtu mmoja utakuja na utaondoka kisha watakuja wengine ndivyo ilivyo


Ukisiliza sauti za wadau wa michezo nyimbo zao ni Yao Yao, Pacome Zouzoua, Max Nzengeli na Mudathir Yahya Abass


Ni walewale mashabiki wa Yanga walioingia hudhuni kuondoka kwa Mayele lakini hali imebadilika sasa hakuna tena msiba ni harusi


Niambie wewe unaenjoy nini kwa Yanga hii?

Post a Comment

0 Comments